Home International CITY YAPIGA MTU KIFURUSHI CHA WIKI

CITY YAPIGA MTU KIFURUSHI CHA WIKI

MANCHESTER City kwenye mchezo wa UEFA Champions League wamemchapa RP Leipzig mabao 7-0.

Uwanja wa Etihad ulisoma hivyo na kuwapa nafasi ya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 8-0.

Ni Erling Haaland alitupia kambani dakika ya 22 kwa mkwaju wa penalti, 24,45,53 na 57 mwamba aliwapa tabu Sana.

Ilkay Gubdogan alitupia dakika ya 49 na Kevin De Bruyne alitupia dakika 90+2.

Katika mchezo huo ni mashuti 23 City walipiga huku 16 yakilenga lango na wapinzani wao walipiga mashuti manne huku moja lililenga lango.

Previous articleKUMBE GEITA GOLD WALIPANGIWA KOSI LA CAF MECHI YA LIGI
Next articleMERIDIANBET YASHUSHA NEEMA KWA BODABODA KAWE