Home Sports SIMBA KAMILI KUIVAA HOROYA KIMATAIFA

SIMBA KAMILI KUIVAA HOROYA KIMATAIFA

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Ally ameweka wazi kuwa mchezo  dhidi ya Horoya utakuwa na ushindani mkubwa ambapo tayari kikosi kimeingia kambini.

“Mchezo wetu utakuwa Jumamosi na tayari kikosi kimeingia kambini kujiandaa na mchezo huo. Jana Jumapili wachezaji walipumzika lakini leo tunaanza rasmi mazoezi.

“Kibu Denis amepona na leo ataanza mazoezi na wenzake. Ni taarifa ya kufurahisha maana kila mmoja anajua ubora wa Kibu na namna alivyoimarika.

“Akili na nguvu zetu tunakwenda kuziweka Jumamosi ili tuweze kushinda na kufuzu Robo Fainali. Ni mechi yenye namna moja pekee tu kushinda. Mechi hii inatukumbusha mechi ya AS Vita, safari hii tupo na Horoya.

“Kila Mwanasimba lazima atambue kwamba tutaingia Uwanja wa Mkapa kwenda kupambana kuingia Robo Fainali. Hatuko tayari kuishia hatua ya makundi na wakati mechi ya kutupeleka robo tutachezea Uwanja wa Mkapa.

“Waamuzi wote wa mchezo wanatokea nchini Misri. Waamuzi hawa wanne watawasili nchini alfajiri ya Machi 17, 2023.Horoya wanatarajiwa kuwasili nchini tarehe Machi 17, 2023 asubuhi,” .

Katika mchezo wa kwanza uliocezwa Guinea Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 ugenini na kuyeyusha pointi tatu mazima.

Previous articleHAT TRICK ZA WAGENI ZIWAZINDUE WAZAWA
Next articleKIKOSI CHA STARS AFCON HIKI HAPA,MBWANA, FEI NDANI