HAT TRICK ZA WAGENI ZIWAZINDUE WAZAWA

  MIPIRA mingi kwenye ligi kwa sasa ni zawadi kwa wageni huku wazawa wakiwa mashuhuda wa jambo hili lazima wazinduke waongeze juhudi.

  Katika idadi ya hat trick tano ambazo zimefungwa kwenye ligi msimu huu ni mzawa mmoja pekee ambaye ni John Bocco yeye kafanya hivyo mara mbili.

  Waliobaki watatu wote ni wachezaji wakigeni hili liwape hasira wazawa kufanya kweli kwenye kufunga na kusepa na zawadi ya mpira.

  Jean Baleke ni ingizo jipya ndani ya Simba, Saido Ntibanzokiza pia hawa wote wamekuwa dirisha dogo la usajili, wazawa wanaocheza ndani ya Simba wanadeni na somo wajifunze.

  Sio Simba tu hata wale ambao wanacheza timu nyingine mbali na Simba ni muhimu kujifunza ili kuongeza ushindani kila wawapo ndani ya uwanja.

  Fiston Mayele wa Yanga ambaye anaongoza kwa idadi ya kufunga mabao naye pia ana hat trick huku wengine wakiwa wanatazama ni muhimu kujifunza na kufanya kwa vitendo kwenye ligi.

  Namna ligi ilivyo ngumu kila kitu kigumu kinapaswa kifanyike na wale wachezaji wageni pamoja na wazawa iwe ni mwendo wa kulipana.

  Mayele na Baleke hawa wote ni kutoka DR Congo huku Ntinbanzokiza akiwa ni kutoka Burundi huku Bongo akiwa ni Bocco peke yake kwa sasa hakika kuna somo la kujifunza.

  Wachezaji wanapenda kufunga pale wanapopata nafasi wafunge kweli ili kuonyesha ubora wao ndani ya ligi inawezekaa.

  Previous articleSINGIDA BIG STARS NGOMA NZITO NA COASTAL UNION
  Next articleSIMBA KAMILI KUIVAA HOROYA KIMATAIFA