YANGA wametumia dakika 10 kuwanyanyua mashabiki wao ndani ya Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.
Ni hatua ya makundi ubao wa Uwanja wa Mkapa unasoma Yanga 1-0 Real Bamako.
Yuleyule Fiston Mayele dakika ya 8 kawatuliza Bamako kwa kufunga bao liliipa uongozi Yanga.
Umakini mdogo kwa Mayele ndani ya dakika 45 za mwanzo umemfanya akamwe kufunga mabao mengine zaidi kwenye mchezo wa leo Machi 8,2023 .