Home Sports MWANA FA:NILIONA MABAO SABA KWA SIMBA

MWANA FA:NILIONA MABAO SABA KWA SIMBA

MWANA FA amesema kuwa aliona nafasi saba za Simba kufunga lakini juhudi zao zilikwama na mwisho mfungaji akawa ni Clatous Chama jambo ambalo ni pongezi kwa timu kupata pointi tatu.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa dakika 90 zilizomsa Simba 1-0 Vipers FC ya Uganda.

Mwana FA amesema:”Niliona namna wachezaji ambavyo mlikuwa mnapambana kusaka ushindi ni mabao saba niliona mlikuwa na nafasi ya kufunga lakini hata wapinzani nao walikuwa na Mungu.

“Mwisho ni bao moja mmefunga hakika mnastahili pongezi na kuendelea kupambana zaidi kwani uwezo mnao na juhudi mnaonyesha,”

Kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan. Simba wamekabidhiwa ahadi yao na ni Mwana FA ambaye ni Naibu Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo jina lake kamili ni Hamis Mwinjuma.

Previous articleKIKOSI CHA YANGA DHIDI YA REAL BAMAKO
Next articleYANGA 1-0 REAL BAMAKO