Home Sports KMC KAMILI KUIKABILI KAGERA SUGAR

KMC KAMILI KUIKABILI KAGERA SUGAR

UOGOZI wa KMC umeweka wazi kuwa upo tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho Machi 9,2023 Uwanja wa Uhuru.

Ni mchezo wa mzunguko wa pili kwa wababe hao kumenyana uwanjani kusaka pointi tatu muhimu.

Rekodi mbaya kwa timu zote mbili zimetoka kufungashiwa virago kwenye Azam Sports Federation.

KMC iliondolewa na Mtibwa Sugar na Kagera Sugar iliondolewa na Mbeya City zote zilifungwa bao mojamoja katika hatua ya 16 bora.

Christina Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo hu.

“Kila kitu kipo sawa na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar,”

Previous articleYANGA 1-0 REAL BAMAKO
Next articleYANGA YAITUNGUA REAL BAMAKO KIMATAIFA