NI moja ya mazao ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Kali Ongala akiwa anaaminika kwenye kikosi cha wale wakubwa wanaoshiriki Ligi Kuu Bara.
Nyota huyo ni Cyprian Kachwele ambaye ni mshambuliaji kutoka kwenye chuo cha kulelea vipaji ndani ya Azam Academy.
Wakati Novemba 15 mwaka huu, akitarajia kutimiza umri wa miaka 16, Kachwele alifunga bao lake la pili la mashindano juzi dhidi ya Mapinduzi FC kwenye Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), akiwa na uzi wa timu kubwa.
Bao la kwanza alifunga pia kwenye michuano hiyo, Azam FC ilipowatungua Malimao FC mabao 9-0.
Kachwele anafuata vema nyayo za washambuliaji waliowahi kupandishwa timu kubwa, Chulunda, Paulm Simchimba na kufanya kweli.