Home Sports SIMBA YAIBUKA NA USHINDI DHIDI YA VIPERS

SIMBA YAIBUKA NA USHINDI DHIDI YA VIPERS

LICHA ya ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 1-0 Vipers bado lile pira Dubai kwa Simba linasakwa kwa tabu sana na ubutu wa ushambuliaji ukiwa ni shida.

Bao pekee la ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi limefungwa na Clatous Chama katika dakika ya 45.

Shukrani kwa Aishi Manula kwa kazi kubwa katika kutimiza majukumu yake akiokoa hatari zilizokuwa zinaindama Simba.

Joash Onyango kwenye ubora wake huku matumizi ya mshambuliaji mmoja yakiwa ni tabu kwa Simba ikiwa Uwanja wa Mkapa.

Pointi sita kibindoni wana kete moja Uwanja wa Mkapa dhidi ya Horoya ambao hawa ni bora kwenye mapigo huru na mpira wa spidi.

Previous articleCHUMA CHA KAZI NDANI YA AZAM FC
Next articleSIMBA HII FA’ MASIHARA NINI, BAMAKO WANACHAKAA