Home Sports YANGA 0-0 PRISONS

YANGA 0-0 PRISONS

DAKIKA 45 za kipindi cha kwanza za msako wa ushindi zimekamilika kwa jasho kwa kila mchezaji kuvuja.

Ni Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la FA wakiwa kwenye msako wa kulitetea taji lao dhidi ya Prisons.

Ubao wa Uwanja wa Azam Complwx unasoma Yanga 0-0 Tanzania Prisons.

Ni Prisons wamepata pigo kutokana na makosa ya mchezaji wao Ibrahim Abraham kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa kumchezea faulo ya kwanza Jesus Moloko na ile ya pili Kisinda ambazo hazikuwa nzuri kwa mujibu wa mwamuzi.

Nyota huyo ameonyeshwa kadi mbili za njano na kufanya atolewe nje kwa kadi nyekundu atakosekana mchezo ujao dhidi ya Namungo mchezo wa ligi.

Previous articleDUBE KAWALIZA KINOMANOMA SIMBA
Next articleGEITA GOLD, SINGIDA BIG STARS ZAPETA