Home Sports DUBE KAWALIZA KINOMANOMA SIMBA

DUBE KAWALIZA KINOMANOMA SIMBA

PRINCE Dube wa Azam FC kwenye msako wa pointi sita dhidi ya Simba katupia mabao mawili, mwendo wa bao mojamoja.

Mzunguko wa kwanza alitupia bao lililoipa pointi tatu na kwenye mchezo wa mzunguko wa pili alitupia bao moja wakapata pointi mojamoja.

Ni pointi nne wamesepa nazo Azam mbele ya Simba ambayo imeambulia pointi moja tu.

Dube amewaliza mashabiki wa Simba kwa kuwa alikuwa mchezaji wa kwanza aliyeifanya Simba kupoteza unbeaten mapema kabisa mzunguko wa kwanza.

Bao lake linashikilia rekodi ya kuwa bao lililofungwa mapema zaidi kwenye ligi sekunde ya 15 mzunguko wa pili.

Previous articleHIKI HAPA KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA PRISONS
Next articleYANGA 0-0 PRISONS