Home Sports MASIKINI MAN UTD IMEJICHOKEA, YAPIGIKA MAGOLI 4-0

MASIKINI MAN UTD IMEJICHOKEA, YAPIGIKA MAGOLI 4-0

Baada ya kuwa na matokeo ya kusuasua katika Msimu wa 2023/24, mambo bado hayajapoa kwa Manchester United ambayo imekubali kichapo cha magoli 4-0 kutoka kwa Crystal Palace kwenye mchezo wa Premier League

Magoli ya Michael Olise (mawili), Jean-Philippe Mateta na Tyrick Mitchell yameifanya Palace kufikisha pointi 43 ikiwa nafasi ya 14 huku Man. United ikibaki nafasi ya Nane ikiwa na pointi 54 ikisaliwa na michezo mitatu kumaliza msimu

Mchezo ujao wa United itakuwa Uwanja wa Old Trafford kuikaribisha Arsenal ambayo ipo kwenye mbio za kuwania ubingwa

Previous articleSIMBA 2-0 TABORA UNITED
Next articleALI KAMWE: AZIZ HAWEZI KUCHEZA NA WATU WANAOFANYA DHULUMA