Home International YANGA NGOMA MPAKA ROBO FAINALI CAF

YANGA NGOMA MPAKA ROBO FAINALI CAF

UONGOZI wa Yanga umewaambia mashabiki kuwa wasiwe na presha ngoma itapigwa mpaka hatua ya robo fainali kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga ipo nafasi ya pili kwenye hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa imekusanya pointi nne kibindoni baada ya kucheza mechi tatu.

Kwenye mchezo dhidi Real Bamako uliochezwa Uwanja wa US du 26 Mars ubao ulisoma Real Bamako 1-1 Yanga.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ameweka wazi kuwa bado wana kazi kubwa ya kufanya kwenye anga za kimataifa wanatambua watatinga hatua ya robo fainali.

“Mwananchi usiwe na mashaka kwa pointi moja ambayo tumepata ugenini sio mbaya ni mwanzo mzuri kwetu nah ii itakwenda kuwekwa historia mpya kwa kutinga hatua ya robo fainali kimataifa.

“Tumedhamiria na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kazi kubwa na ngumu hasa kwa mechi zetu mbili Uwanja wa Mkapa tuna pambana kupata pointi sita ili kusonga mbele hapo hesabu zitajibu.

“Ninaona wapo ambao wameanza kukata tamaa kwa kushika tama hilo wasiwe nalo kabisa, Wananchi watembee kifua mbele tunafanya kazi kubwa kufikia malengo yetu lazima tushirikiane,” .

Previous articleEL CLASICO NI CLASSIC
Next articleSINZA MPO? MERIDIANBET IMEWALETEA DUKA LA KUBETIA NJOONI KWA WINGI MBASHIRI