Home Sports HILI KUBWA LA M 5, MSIMBAZI WATOA SHUKRANI

HILI KUBWA LA M 5, MSIMBAZI WATOA SHUKRANI

BAADA ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kuweka wazi kuwa atanunua bao la timu za Tanzania zinazoshiriki mashindano ya kimataifa kwa milioni 5, uongozi wa Simba umetoa shukrani za dhati kwa jambo hilo.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa jambo hilo ni kubwa lakini wao hawatafunga kwa ajili ya fedha bali kupokea oda kutoka kwa kiongozi huyo anayependa maendeleo ya Tanzania.

“Hatutafunga mabao kwa ajili ya milioni licha ya kuwa ni fedha nzuri hizo zinakuwa ni motisha kwa wachezaji ambao wanajua wajibu wao kwenye kazi na hasa kwenye mashindano ya kimataifa.

“Milioni 5 kwa kila goli. Tunakushukuru jemedari wetu, Rais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutuongezea hamasa. Vijana wako imara na hamasa yako imekuja muda muafaka.

“Klabu ya Simba tunatambua mchango mkubwa wa Serikali kwenye kuendeleza michezo. Na ndio maana tuliamua kuiweka nchi mbele kwa kutangaza vivutio vyetu vya utalii,” .

Simba Februari 18 2023 inatarajiwa kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.

Jumapili Februari 19 itakuwa ni Yanga dhidi ya TP Mazembe unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Hivyo mwanja huo wa m 5 kwa kila bao sio Simba tu watahusika ikiwa watafunga bali hata kwa Yanga ni mwendo wa m 5.

 

Previous articleROBERTINHO APATA DAWA YA RAJA CASABLANCA
Next articleSHIKENI UKWELI,MECHI ZIJAZO NI NGUMU KWA SIMBA NA YANGA