Home Sports SHIKENI UKWELI,MECHI ZIJAZO NI NGUMU KWA SIMBA NA YANGA

SHIKENI UKWELI,MECHI ZIJAZO NI NGUMU KWA SIMBA NA YANGA

Anaandika Jembe

SIMBA na Yanga zimepoteza mechi za kwanza za ugenini kimataifa.

Tukubali timu zetu zilijiandaa lakini Caf CL na Caf CC si lelemama, si sehemu ya maneno mengi na kupeana moyo tu…NI MAPAMABO HALISI…

Simba wamefungwa na Horoya wanayoizidi kwenye ubora wa Rank za Caf, hali kadhalika Yanga kwa Monastir.

Sasa nyumbani wanakwenda kukutana na wenye rank za juu Afrika. TP Mazembe au Raja haiwezi kuwa LELEMAMA.

Niliwaambia achaneni na zile hadithi sijui tunaweza Tunisia maana Nabi anatokea huko au zile za TP Mazembe wameisha.

Lazima kujipanga upya na kuhakikisha wageni wanaacha pointi zote nyumbani lakini lazima kuzipa nguvu timu.

Niwaambie, SI LAZIMA TUSIKILIZE UONGO ndio.tunaweza KUSIKILIZA UKWELI NA TUKAUELEWA halafu mapambano YAKAWA SAHIHI ZAIDI.

Mechi zijazo NI NGUMU ZAIDI YA TULIZOPOTEZA lakini inawezekana kabisa KUWALAZIMISHA WAGENI KUACHA POINTI ZOTE TANZANIA.

Previous articleHILI KUBWA LA M 5, MSIMBAZI WATOA SHUKRANI
Next articlePIA PREMIUM MZUKA MPYA WA KASINO YA MTANDAONI MERIDIANBET