Home International WANANCHI WAANZA SAFARI KUIWAHI TP MAZEMBE

WANANCHI WAANZA SAFARI KUIWAHI TP MAZEMBE

BAADA ya kete ya kwanza kukamilika huku wakipoteza mchezo wao kikosi cha Yanga kimeanza safari kurejea Dar.

Wawakilishi hao kwenye Kombe la Shirikisho Afrika walikamilisha dakika 90 na ubao ukasoma US Monastir 2-0 Yanga.

Msafara wa wachezaji na benchi la ufundi unatarajiwa kuwasili nchini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao ujao dhidi ya TP Mazembe.

Miongoni mwa nyota ambao walikuwa kwenye mchezo huo na wapo kwenye msafara ni pamoja na Aziz KI, Kibwana Shomary, Fiston Mayele, Dickson Job.

Jumapili Yanga inatarajiwa kumenyana na TP Mazembe, Uwanja wa Mkapa.

Ni Februari 19 Yanga inatarajia kumenyana na vnara hao kwenye kundi D baada ya kuwatungua mabao 3-1 Real Bamako.

Previous articleKIUNGO HUYU MGUMU AIPASUA KICHWA SIMBA
Next articleLIGI YA MABINGWA KITAWAKA PSG vs BAYERN MUNICH PATA ODDS BOMBA KUTOKA MERIDIANBET