Home International REAL MADRID WAWEKA REKODI YA KUTWAA MATAJI

REAL MADRID WAWEKA REKODI YA KUTWAA MATAJI

REAL Madrid ni mabingwa baada ya kushinda kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia la Klabu, wakilitwaa taji hilo mara tano wakiwa na rekodi tamu ya kusepa na taji hilo mara nyingi zaidi.

Real Madrid ilipata ushindi wa mabao 5-3 dhidi ya Al Hilal ya Saudia ambao walikwama kutimiza malengo yao kwenye mtanange huo.

Mabao ya Real Madrid yamepachikwa kimiani na Vini Jr alitupia kambani mara mbili dakika ya 13 na 69, Federico Valverde pia mawili dakika ya 18 na 58 na kamba moja ilijazwa kimiani na Karim Benzema dakika ya 54.

Mabao ya Al Hilal yalifungwa na Moussa Marega dakika ya 26 na Luciano Vietto dakika ya 63 na 73 ngoma ilipigwa Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, Morocco.

Previous articleVIDEO:KUMBE YANGA WAMEFANYIWA FIGISU
Next articleHIKI HAPA KIKOSI CHA YANGA DHIDI YA US MONASTIR