Home Uncategorized YANGA YAWEKA REKODI MATATA IKIWATUNGUA NAMUNGO

YANGA YAWEKA REKODI MATATA IKIWATUNGUA NAMUNGO

YANGA imesepa na pointi tatu mazima mbele ya Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Yanga 2-0 Namungo FC.

Kila kipindi Yanga walitupia bao moja dakika ya 43 ni Dickson Job na kipindi cha pili ni Aziz KI alitupia bao kwenye mchezo huo.

Ilikuwa ni dakika ya 63 bao hilo alipachika baada ya makosa ya safu ya ulinzi ya Namungo kwenye harakati za kuokoa hatari.

Ushindi huo unaifanya Yanga kuandika rekodi mpya yakushinda mechi 9 mfululizo ikivunja rekodi iliyowekwa na Azam FC ambayo haikufungwa kwenye mechi 8 na iliwatungua Simba pia.

Pia Yanga imeshinda mechi hizo huku ikikusanya clean sheet nane kwa kipa wao namba moja Diarra Djigui ambaye wanamuita mdaka mishale.

Kibindoni imekusanya pointi 59 baada ya kucheza mechi 22 za ligi.

Previous articleSIMBA WAJA NA MTOKO WA FAMILIA
Next articleAZAM YAPOTEZA MBELE YA DODOMA JIJI