Home Uncategorized SIMBA WAJA NA MTOKO WA FAMILIA

SIMBA WAJA NA MTOKO WA FAMILIA

BAADA ya ushindi wa mabao 3-1 waliopata dhidi ya Singida Big Stars kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, kesho Simba wanatarajia kumenyana na Al Hilal.

Mchezo huo ambao Simba watajitupa kesho Uwanja wa Mkapa ni wa kimataifa wa kirafiki ikiwa ni maandalizi ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua utakuwa mchezo wenye ushindani lakini burudani itakuwepo.

“Ni mtoko wa familia baada ya ule tuliocheza ugenini wakati tulipokwenda nao kushuhudiwa na mashabiki wengi hivyo ni muda wa mashabiki wetu kujitokeza.

“Huu ni mtoko kwa maana hiyo hata kiingilio ni rafiki kuanzia kwa wale watoto chini ya miaka 10 itakuwa bure hata wakiwa 50 wataingia wazazi na walezi njooni najua mmetoka kutazama burudani dhidi ya Singida Big Stars huu ni mtoko,” amesema.

Florent Ibenge, Kocha Mkuu wa Al Hilal amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu na watafanya kazi kubwa kupata ushindi.

Previous articleMATHEO ANTHONY KUIKOSA RUVU SHOOTING
Next articleYANGA YAWEKA REKODI MATATA IKIWATUNGUA NAMUNGO