Home Sports MATHEO ANTHONY KUIKOSA RUVU SHOOTING

MATHEO ANTHONY KUIKOSA RUVU SHOOTING

MATHEO Anthony, nyota wa KMC kesho anatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri,Morogoro saa 10:00 jioni.

Sababu za nyota huyo kuukosa mchezo huo ni kutokuwa fiti baada ya kupata maumivu.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting lakini watakosa huduma ya nyota huyo.

KMC imetoka kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Namungo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma KMC 1-3 Namungo ambapo Namungo walisepa na pointi tatu mazima huku Ibrahim Mukoko akisepa na mpira baada ya kufunga hat trick.

Previous articleVIDEO:TUNDA AWACHAMBUA CHAMA,SAKHO,BALEKE
Next articleSIMBA WAJA NA MTOKO WA FAMILIA