SportsMANULA KATUNGULIWA SIMBA IKISEPA NA POINTI TATU Saleh3 years ago3 years ago01 mins KIUNGO wa Simba Pape Sakho amefunga bonge moja ya bao dhidi ya Singida Big Stars dakika ya 63. Bao hilo linafanya ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 3-1 Singida Big Stars. Mabao mawili ya awali kwa Simba ni mali ya Jean Baleke aliyepachika bao mapema dakika ya 8 na lile la pili ni mali ya Saidi Ntibanzokiza dakika ya 20. Singida Big Stars bao lao matata na zuri limefungwa na Bruno Gomez dakika ya 34 kwa pigo la faulo lilimshinda Aishi Manula. Manula hakuwa na bahati na Gomez ambaye amefunga mabao 9 ndani ya Ligi Kuu Bara. Gomez kazitungua timu 8 ambapo kwenye mechi saba zote Singida Big Stars ilikuwa inasepa na ushindi lakini leo ngoma imekuwa nzito. Post navigation Previous: AZAM FC WATUA NDANI YA DODOMANext: YANGA KAMILI KUIVAA NAMUNGO
Soccer Football - International Friendly - Spain v Brazil - Santiago Bernabeu, Madrid, Spain - March 26, 2024 Spain's Rodri scores their third goal from the penalty spot REUTERS/Violeta Santos Moura Je Fainali ya Kombe la Dunia 2026 Itakuwa Brazil vs Hispania? Saleh2 days ago 0