Home Sports KMC YATINGA 16 BORA KOMBE LA SHIRIKISHO

KMC YATINGA 16 BORA KOMBE LA SHIRIKISHO

NYOTA wa KMC, Emmanuel Mvuyekule mshuti wake akiwa nje ya 18 umewapa faida mashabiki wa timu hiyo na kunyanyuka kwenye viti.

Ni kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho raundi ya tatu ambapo ubao wa Uwanja wa Uhuru umesomaKMC 1-0 COPCO.

Bao hilo lilipachikwa dakika tano zikiwa zimesalia kugota dakika ya 90 baada ya dakika 84 kumeguka bilakufungana.

Mbali na KMC kuibuka na ushindi huo na kutinga hatua ya 16 bora Singida Big Stars wao wamewatungua Ruvu Shooting mabao 2-1 ukiwa ni mchezo uliokusanya mabao mengi Januari 28 kwenye Kombe la Shirikisho.

Previous articleKOMBE LA FA SIMBA 0-0 COASTAL UNION
Next articleSIMBA YATINGA 26 BORA MBELE YA COASTAL UNION