Home Sports HIZI HAPA ZIMETINGA 16 BORA

HIZI HAPA ZIMETINGA 16 BORA

KOMBE la Shirikisho Azam Sports Federation limezidi kuunguruma ambapo leo kuna mechi zitachezwa kusaka zile ztakazoshinda kutinga hatua ya 16 ora.

Miongoni mwa mechi ambazo zinatarajiwa kuchezwa leo ni pamoja na Simba dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkapa.

Kwa mechi ambazo zilichezwa jana, Januari 27, matajiri wa Dar, Azam FC walishusha kichapo kwa Dodoma Jiji huku nyota wao mpya Stephen Sey  akikosa penalti kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Matokeo yalikuwa namna hii:-Azam FC 4-1 Dodoma Jiji
Mtibwa Sugar 4-0 Buhaya FC
Green Warrior 2-1 Mbuni FC
Polisi Tanzania 1-1 JKT Tanzania (Pen 4-5)

Timu zilizofanikiwa kutinga hatua ya 16 bora kwenye mechi za Januari 27 ni: Azam FC, Mtibwa Sugar, Green Warriors na JKT Tanzania na mabingwa watetezi wa taji hilo ni Yanga ambao watacheza kesho na Rhino.

Previous articleNATHAN AKE APELEKA KILIO KWA WASHIKA BUNDUKI
Next articleBOSI MAN U ANAFIKIRIA MATAJI