Home Uncategorized NATHAN AKE APELEKA KILIO KWA WASHIKA BUNDUKI

NATHAN AKE APELEKA KILIO KWA WASHIKA BUNDUKI

BAO pekee ambalo lilipeleka kilio kwa washika bunduki Arsenal kwenye mchezo wa raundi ya 4 FA Cup lilipachikwa kimiani na nyita Nathan Ake.

Kwenye mchezo huo uliokuwa unaushindani mkubwa mashabiki wa Arsenal walishuhudia dakika 45 ngoma ikiwa ni nzito kwa timu zote mbili wakiamini watafanya jambo.

Ubao ulipabdilika usomaji dakika ya 64 ambapo ulisoma Manchester City 1-0 Arsenal na ilikuwa hivyo mpaka mwisho wa mchezo na mtupiaji akiwa ni Ake.

Kwenye mchezo huo Arsenal walipiga jumla ya mashuti matano kuelekea langoni mwa wapinzani na ni mashuti mawili yalilenga lango huku City wakipiga mashuti 8.

Katika mashuti 8 ya City ni mashuti matatu yalilega lango ikiwa ni pamoja na bao la ushindi lililowapeleka hatua ya tano ya FA.

Previous articleCEO SIMBA AANZA NA NYUNDO 5, NABI AFANYA MAAMUZI MAZITO
Next articleHIZI HAPA ZIMETINGA 16 BORA