Home Uncategorized MWENDO WA POLISI TANZANIA UNAFIKIRISHA

MWENDO WA POLISI TANZANIA UNAFIKIRISHA

MWENDO wake kwa msimu wa 2022/23 wa Polisi Tanzania sio wa ligwaride songa mbele bali ni ligwaride rudi nyuma ikiwa unafikirisha kwelikweli.

Januari 14 ikiwa ugenini, ubao wa Uwanja wa Majaliwa ulisoma Namungo 0-2 Polisi Tanzania na walikamilisha dakika 90 wakiwa pungufu.

Kwenye mchezo huo mchezaji wao mmoja alionyeshwa kadi nyekundu wakati wakiongoza bao moja mbele ya Wauaji wa Kusini.

Wakaibuka na ushindi kwa mabao ya ingizo lao jipya Henock ambaye alitupia mabao yote.

Wakiwa wanaamini kasi yao itaendelea mbele ya Geita Gold, wakasepa na pointi moja wakiwa ugenini.

Ilikuwa Januari 20, ubao wa Uwanja wa Nyankumbu ulisoma Geita Gold 1-1 Polisi Tanzania.

Ni nafasi ya 15 kwenye msimamo na pointi zake ni 15 msimu wa 2022/23 baada ya kucheza mechi 21.

Timu hiyo ipo chini ya Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera ambaye ameweka wazi kwamba timu hiyo haitashuka daraja.

“Unadhani Polisi Tanzania itashuka daraja? Hapana kila kitu kitakuwa sawa na matokeo yatapatikana,”.

Hello Polisi Tanzania kulikoni na mwendo huu?

Previous articleNAMUNGO KAMILI KUIKABILI KMC
Next articleSIMBA KUKIPIGA DHIDI YA AL HILAL YA SUDAN KWA MKAPA