Home Sports SIMBA KUKIPIGA DHIDI YA AL HILAL YA SUDAN KWA MKAPA

SIMBA KUKIPIGA DHIDI YA AL HILAL YA SUDAN KWA MKAPA

KLABU ya Al Hilal ya nchini Sudan kesho Januari 25,2023 inatarajiwa kuwasili nchini Tanzania kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiandaa na michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kutokana na mahusiano mazuri ambayo wamejenga dhidi ya Klabu ya Simba SC ya Tanzania hawa watatakuwa wenyeji wao.

Wakiwa nchini watacheza michezo mitatu ya kirafiki dhidi ya Simba SC, Azam FC na Namungo FC. Mchezo wao dhidi ya wenyeji wao Simba utakuwa wa mwisho na utachezwa Februari 5, 2023 kwenye Uwanja wa Mkapa.

Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtanza Mangungu ameweka wazi kuwa haya ni matokeo ya kuwa na mahusiano mazuri na timu nyingine ndani na nje ya nchi.

Ikumbukwe kwamba timu hiyo iliweka kambi ya wiki moja nchini Dubai na kwa sasa imerejea Dar kuendelea na mipango kazi.

Mchezo ujao kwa Simba inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ni dhidi ya Coastal Union ambao ni wa Kombe la Shirikisho unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Januari 28,2023.

Previous articleMWENDO WA POLISI TANZANIA UNAFIKIRISHA
Next articleMTAMBO WA MABAO AZAM UNAREJEA MDOGOMDOGO