Home Sports NAMUNGO KAMILI KUIKABILI KMC

NAMUNGO KAMILI KUIKABILI KMC

MCHEZO uliopita Namungo FC iliyeyusha pointi tatu mazima ikiwa nyumbani.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Majaliwa ulisoma Namungo 0-2 Polisi Tanzania.

Leo Januari 24 kikosi hicho kina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya KMC yenye maskani yake Kinondoni.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru.

Nyota Shiza Kichuya ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya kila mechi kusaka ushindi kwa ajili ya timu.

Kwenye msimamo Namungo imekusanya pointi 26 ikiwa nafasi ya sita baada ya kucheza mechi 20 inakutana na KMC yenye pointi 23 nafasi ya 10.

“Kila mchezo kwetu ni muhimu na ambacho tunahitaji ni pointi tatu inawezekana kutokana na mipango kazi yetu.

“Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwa kuwa tunahitaji kushinda ili kuwapa furaha nasi furaha yetu ipo kwenye ushindi,”.

Previous articleMCHEZO WA KIPA SIMBA KUBUMA AZAM FC HUYU HAPA MTIBUAJI
Next articleMWENDO WA POLISI TANZANIA UNAFIKIRISHA