MTAMBO WA MABAO AZAM UNAREJEA MDOGOMDOGO
KWENYE chati ya ufungaji mabao ndani ya Azam FC, Idris Mbombo ni namba moja akiwa ametupia mabao 7 kibindoni. Nyota huyo ni imara kwenye mapigo huru ikiwa ni pamoja na penalti aliwahi kuwatungua Ruvu Shooting bao moja Uwanja wa Mkapa. Hakuwa kwenye mwendelezo wake bora kutokana na kutokuwa fiti lakini kwa sasa ameanza kurejea mdogomdogo….