Home International ARSENAL NI MOTO KWELIKWELI

ARSENAL NI MOTO KWELIKWELI

KASI ya Arsenal kwenye Ligi Kuu England ni moto baada ya kupindua meza kwenye mchezo dhidi ya Manchester United wakiwa nyumbani.

Ubao wa Uwanja wa Emirates umesoma Arsenal 3-2 Manchester United ambao walipigiwa mpira mkubwa wakiwa ugenini.

Ni Marcus Rashford alianza kufunga dakika ya 17 na lile la pili kwa United lilifungwa na Lisandro Martinez daika ya 59.

Ni Edie Nketiah alipeleka maumivu United wa kufunga bao la ushindi dakika ya 90 huku lile la usawa alifunga dakika ya 24 na bao lingine limefungwa na Bukayo Saka dakika ya 53.

Ni pointi 50 kibindoni wakiwa nafasi ya kwanza United nafasi ya nne na pointi 39.

Previous articleBALEKE, SAWADOGO WAFANYA BALAA SIMBA
Next articlePIRA HILI KUTOKA YANGA RUVU KUKUTANA NALO