Home Sports PIRA HILI KUTOKA YANGA RUVU KUKUTANA NALO

PIRA HILI KUTOKA YANGA RUVU KUKUTANA NALO

WAKATI Simba wakitamba kupiga pira Dubai kutokana na kambi yao ya wiki moja waliyoweka huko, vinara wa Ligi Kuu Bara Yanga wametamba kuwapigia pira popcon wapinzani wao Ruvu Shooting.

Leo Uwanja wa Mkapa, Yanga watawakaribisha Ruvu Shooting kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga ilishinda kwa mabao 2-1 hivyo leo Ruvu watakuwa wanahitaji kuvunja mwiko huyo wakati Yanga wakipambana kulinda rekodi yao.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kuwakabili Ruvu Shooting na watawaigia pira popcorn.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuona namna ambavyo tutakuwa na kazi kubwa na nzuri kwenye kusaka pointi tatu ambapo tutacheza pira popcorn mbele ya wapinzani wetu.

“Tumekuwa na rekodi bora kwenye mechi za hivi karibuni jambo ambalo linatufanya tusiwe na mashaka kwenye mechi tunazocheza kikubwa ni kuzidi kujenga hali ya kujiamini na kucheza kwa nidhamu,” amesema Kamwe.

Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 53 inakutana na Ruvu Shooting yenye pointi 14 zote zimecheza mechi 20 msimu huu.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema wapo tayari kwa mchezo dhidi ya Yanga watapambana kupata pointi tatu.

Previous articleARSENAL NI MOTO KWELIKWELI
Next articleYANGA YAMUANDIKIA BARUA FEI TOTO, WATAALAMU KUJADILI KIDOGO