Home Sports MTAMBO WA MABAO SIMBA KUIKOSA DODOMA JIJI

MTAMBO WA MABAO SIMBA KUIKOSA DODOMA JIJI

KUELEKEA kwenye mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara kati ya Dodoma Jiji dhidi ya Simba, nyota wa timu hiyo Clatoous Chama hatakuwa sehemu ya kikosi.

Chama ni namba moja kwenye kutengeneza pasi za mabao akiwa ametoa asi 12 na kufunga mabao matatu.

Kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mbeya City nyota huyo alitoa pasi moja ya bao kwa mshikaji wake Saidi Ntibanzokiza ambaye alipachika bao hilo dakika ya 19.

Kwa mujibu wa Juma Mgunda, kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa  Chama kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City alikuwa anacheza akiwa anasumbuliwa na Malaria pamoja na mafua.

Alipoyeyusha dakika 33 benchi la ufundi likaona inatosha na hayupo kwenye msafara wa Simba uliopo kwa wakulima Zabibu, Dodoma.

“Chama alikuwa anaumwa na kwenye mchezo wetu dhidi ya Mbeya City alikuwa anasumbuliwa na mafua pamoja na Malaria hivyo dakika 33 alizopewa mwalimu aliona zinamtosha na hakutaka kumuongezea mzigo mzito.

“Kwa sasa anaendelea na program hatupo naye kwenye msafara kutokana na kutokuwa fiti sio yeye tu hata Banda, (Peter) Inanga, (Henock) naye hayupo fiti hivyo hatakuwa sehemu ya mchezo,”.

Kesho Januari 22 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma kwa timu hizo kuwa kwenye msako wa pointi tatu.

Previous articleNYOTA HUYU WA DODOMA JIJI TARATIBU ANAKUJA
Next articleMUONEKANO WA UKURA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI