Home Sports JEMBE JIPYA MTIBWA SUGAR LAANZA KAZI

JEMBE JIPYA MTIBWA SUGAR LAANZA KAZI

INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar Vitalis Mayanga ataonekana ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani akitumia jezi namba 27.

Alikuwa anakipiga ndani ya Polisi Tanzania anaanza changamoto mpya ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar kinachonolewa na Kocha Mkuu, Salum Mayanga.

Mshambuliaji huyo msimu uliopita hakuwa kwenye mwendo bora ndani ya kikosi cha Polisi Tanzania baada ya kupata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Simba uliokuwa ni wa ligi.

Tayari ameanza kurejea mdogomdogo akiendelea kutimiza majukumu yake ambapo atakuwa Morogoro.

Ikumbukwe kwamba aliwahi kucheza Ndanda na KMC ambapo huko hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza.

Previous articleNABI AWACHAMBUA MAYELE, MUSONDA,MFUMO WABADILISHWA SIMBA
Next articlePUMZIKA KWA AMANI BANDA, UMAKINI UONGEZEKE KUOKOA NGUVU KAZI