Home Sports PUMZIKA KWA AMANI BANDA, UMAKINI UONGEZEKE KUOKOA NGUVU KAZI

PUMZIKA KWA AMANI BANDA, UMAKINI UONGEZEKE KUOKOA NGUVU KAZI

PUMZIKA kwa amani Mohammed Banda, uangalizi zaidi kwa timu za vijana unahitajika kuokoa wengine.

Ni pigo kwenye ulimwengu wa michezo Bongo lakini ni muhimu pia kuongeza umakini kwenye eneo la vijana kutokana na matatizo haya kutokea

Januari 19,2023 Uongozi wa Singida Big Stars ulitoa taarifa kuhusu kutangulia mbele za haki kwa kijana Banda.

Taarifa hiyo ilisomekana hivi:”Tunathibitisha kutokea kwa kifo cha aliyekuwa mchezaji na kapteni wa timu yetu ya vijana (U17), Mohammed Banda, kilichotokea leo asubuhi Januari 19, 2023.

“Banda alipoteza maisha alipofikishwa Hospitali ya Mkoa wa Singida baada ya kugongana kichwani na mchezaji mwenzake wakiwa mazoezini katika Uwanja wa Magereza, Singida.

“Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mzito na kuwa ni pigo,”.

Ikumbukwe kwamba 2016 katika Ligi Kuu ya Vijana U 20 mchezaji wa Mbao Ismail Khalfan alifariki dunia Uwanja wa Kaitaba, Kagera pia Mshauri Salim wa Coastal Union U 20 alifariki dunia Uwanja wa Mkwakwani.

Mazingira ya vijana pamoja na benchi la ufundi ni muhimu kuboresha ili kupunguza maumivu haya na nguvu kazi ya Tanzania.

Previous articleJEMBE JIPYA MTIBWA SUGAR LAANZA KAZI
Next articleCHAMA ATOA TAMKO SIMBA, BEKI MPYA YANGA ANATUA LEO