Home Uncategorized SIKU MBAYA KAZINI KWA IHEFU

SIKU MBAYA KAZINI KWA IHEFU

SIKU mbaya kazini kwa mastaa wote wa Ihefu pamoja na benchi la ufundi baada ya mbinu zao zote kufeli mbele ya Yanga ndani ya dakika 90.

Benchi la ufundi likiwa limewaanzisha washambuliaji wake Obrey Chirwa na Adam Adam ambaye ni ingizo jipya kutoka Mtibwa Sugar walishuhudia dakika 90 zikayeyuka bila shuti lililolenga lango.

Kipa Diarra Djigui wa Yanga hakuwa na kazi kubwa mbele ya Ihefu ambao walikuwa wanacheza kwa kujilinda na walikuwa wanaonekana wanahitaji sare ngoma ikawageukia.

Ni kadi moja ya njano alionyeshwa nyota wa Ihefu, Chirwa dakika ya 42 na shuti lake la dakika ya 17 halikulenga lango.

Hata walipoingia washambuliaji wengine ikiwa ni pamoja na Andrew Simchimba na Rashid Juma ngoma ilikuwa nzito walikutana na ukuta chuma wa Yanga chini ya Bakari Mwamnyeto.

Kipa Fikirini Bakari atabaki kujilaumu mwenyewe kwa kuwa kazi kubwa alifanya kipindi cha kwanza kipindi cha pili akadhani anacheza peke yake uwanjani, hapo anapaswa kujifunza kuwa imara zaidi.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza Uwanja wa Highland Estate, ubao ulisoma Ihefu 2-1 Yanga hivyo ulikuwa ni mchezo wa kisasi

Previous articleMUDHATHIR MCHEZO WAKE WA KWANZA KATEMBEZA MIKATO
Next articleSIMBA WAREJEA KUAANZA NA MBEYA CITY KWA MKAPA