Home Sports MUDHATHIR MCHEZO WAKE WA KWANZA KATEMBEZA MIKATO

MUDHATHIR MCHEZO WAKE WA KWANZA KATEMBEZA MIKATO

ALIWATEMBEZEA mikato Ihefu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara Januari 16,2023 mpaka mwamuzi akaonekana kumwambia hili ni onyo la mwisho ukizingua adhabu inakuhusu.

Ni Mudhathir Yahya kwenye kiwango kizuri dhidi ya Ihefu ambao walikuwa wanajilinda muda wote na mwisho wakapoteza kwa kufungwa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Fiston Mayele.

Kiungo huyo mkabaji alikuwa akicheza kwa ushirikiano na wachezaji wengine huku akiwa na mshikaji wake wa karibu Sure Boy waliyecheza pamoja ndani ya Azam FC.

Kazi kubwa kwa wachezaji wakati huu wa mzunguko wa pili iwe ni kucheza kwa nidhamu na kuacha ile mikato ya kimyakimya isiyo ya lazima.

Itakumbukwa kwamba Muda alimchezea faulo zote mbili mshambuliaji wa Ihefu Adam Adam ilikuwa dakika ya 9 na 37 kwenye mchezo huo.

Mbali na Mudha ambaye ni ingizo jipya akiwa ni mchezaji huru pia Kenned Musonda naye alipata nafasi ya kucheza kwenye mchezo huo.

Ni jezi namba 25 kakaidhiwa Musonda ambaye ni mshambuliaji kutoka Power Dynamo.

Previous articleUBORA WA WACHEZAJI WAIPONZA TANZANIA PRISONS
Next articleSIKU MBAYA KAZINI KWA IHEFU