Home Sports UBORA WA WACHEZAJI WAIPONZA TANZANIA PRISONS

UBORA WA WACHEZAJI WAIPONZA TANZANIA PRISONS

“TATIZO ni ubora wa wachezaji kwa wapinzani wetu jambo ambalo limetugharimu, ” maneno ya Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Patrick Odhiambo baada ya ubao wa Uwanja wa Azam Complex kusoma Azam FC 3-0 Prisons.

Mchezo huo wa ligi ulitawaliwa na tambo za kutosha kwa pande zote mbili zikiweka wazi kwamba ni pointi tatu wanahitaji na mwisho zikasalia Azam Complex.

Prisons walianza kujivuruga baada ya bao la kujifunga mapema dakika ya 5 kupitia kwa Yona Amos kisha mvua ya mabao ilisimama mpaka muda wa mapumziko kwa kuwa ulikuwa unasoma Azam FC 1-0 Prisons.

Kipindi cha pili dakika tatu mbele Azam FC ilipachika bao la pili kupitia kwa Abdul Suleiman, dakika 48 na lile la tatu lilipachikwa na Kipre Junior dakika ya 70.

Azam FC inafikisha pointi 43 ikiwa nafasi ya tatu na Prisons nafasi ya 11 pointi zake ni 21.

Previous articleMZIKI UMETIMIA, MAYELE AMESHINDIKANA
Next articleMUDHATHIR MCHEZO WAKE WA KWANZA KATEMBEZA MIKATO