Home Sports YANGA KUWAKABILI MASHUJAA KIGOMA

YANGA KUWAKABILI MASHUJAA KIGOMA

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga leo watakuwa kwenye msako wa pointi tatu dhidi ya Mashujaa Uwanja wa Lake Tanganyika.

Ipo wazi kwamba Yanga ni namba moja kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 62 baada ya kucheza mechi 24. nafasi ya pili ni Azam FC wenye pointi 54 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu na pointi 50.

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wanatambua kazi ni kubwa mbele ya Mashujaa lakini watafanya jitihada kupata ushindi.

“Kila mchezo kwetu ni muhimu kupata pointi tatu mashabiki wanatambua kwamba furaha kubwa ipo kwenye ushindi hilo hata wachezaji wanajua pia.

“Kikubwa ni kujitokeza kwa wingi na wachezaji kujituma kutumia nafasi ambazo tutazipata kwenye mchezo wetu, tupo tayari na tunaamini kazi itakuwa nzuri.”

Mashujaa ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi 24.

Previous articleSuka Jamvi Lako Leo na Meridianbet
Next articleANAONDOKA NDANI YA SIMBA KIUNGO HUYU MGUMU