Home Sports DIRECTOR KHALFANI AFARIKI LEO HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

DIRECTOR KHALFANI AFARIKI LEO HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

Muongozaji wa video za muziki nchini Tanzania ‘Director Khalfani Khalmandro’ amefariki Dunia leo asubuhi  Mai 5, 2024 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Taarifa zilieleza kuwa Khalfani alilazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, taasisi ya mifupa MOI akiwa na tatizo la damu kuvilia kwenye ubongo lililopelekea changamoto ya kupooza upande wake wa kulia wa mwili.

Enzi za Uhai wake alijipatia umaarufu kwa kuongoza Video za Wasanii kama Aslay, NavyKenzo, Christian Bella, Baby Madaha, Chinbees, Shilole na Linah

Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wapenzi wote wa sanaa ya Director Khalfani katika nyakati hizi ngumu!

Inna Lillahi wa inna ilayhi raji’un

Previous articleNYOTA WA SIMBA WANAPITIA KATIKA HALI YA KUPANDA NA KUSHUKA
Next articleSuka Jamvi Lako Leo na Meridianbet