Home Sports MABINGWA WAPYA WA KOMBE LA MAPINDUZI NI MLANDEGE

MABINGWA WAPYA WA KOMBE LA MAPINDUZI NI MLANDEGE

MLANDEGE kutoka Zanzibar ni mabingwa wa Mapinduzi Cup 2023 baada ya kuitingua Singida Big Stars kwenye hatua ya fainali Uwanja wa Amaan.

Ni ushindi wa mabao 2-1 walipata kwenye fainali iliyokuwa na ushindani mkubwa.
Mabao kwenye mchezo huo yalifungwa na Bashima Saile dakika ya 7 na lile la ushindi lilifungwa na Abdulnassir Mohamed dakika ya 19.

Hivyo Mlandege wao walimaliza kazi ndani ya dakika 45 za mwanzo na kipindi cha pili walirejea kujilinda zaidi.

Bao la Singida ig Stars lilifungwa na Francy Kazad dakika ya 51 akitumia makosa ya mabeki wa timu hiyo kwenye kuokoa hatari lakini hakufanikiwa kuipa ubingwa timu hiyo.
Anafikisha mabao 7 akiwa ni kinara wa utupiaji kwenye Mapinduzi 2023.

Ikumbukwe kwamba Mlandege hawa waliwavua ubingwa Simba kwenye hatua ya makundi kwa kuitungua bao 1-0.

Hongera mabingwa wapya wa Mapinduzi 2023, Mlandege

Previous articleJEMBE JIPYA MTIBWA SUGAR LATIMIZA NDOTO
Next articleKIUNGO LUIS AKUBALI KUTUA YANGA, OFA YA MAANA MEZANI