Home Sports KIUNGO LUIS AKUBALI KUTUA YANGA, OFA YA MAANA MEZANI

KIUNGO LUIS AKUBALI KUTUA YANGA, OFA YA MAANA MEZANI

TAARIFA zikufikie kuwa, kiungo wa Al Ahly ya nchini Misri, Luis Miqquissone ameikubali ofa nono aliyowekewa na mabosi wa Yanga ili kufanikisha dili lake la kutua mitaa ya Jangwani.

Luis ni kati ya wachezaji wanaotajwa kuwaniwa na Yanga katika usajili huu wa dirisha dogo lililofunguliwa tangu Desemba 16,2022.

Wachezaji wanaotajwa kuwepo katika mipango ya kusajiliwa na Yanga hadi hivi sasa ni kiungo wa Vipers FC, Bobosi Byaruhanga, winga wa RS Berkane ya nchini Morocco, Chadrack Muzungu na Luis mwenyewe.

Chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga, kimeliambia Championi Jumamosi kuwa, kiungo huyo yupo tayari kujiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka mitatu wenye thamani kubwa ambayo ni siri.

Kilisema kuwa ofa waliyoitoa Yanga inakadiliwa kufikiwa zaidi ya Sh 500Mil ili kukamilisha usajili wake, licha ya mkataba wake kuwa na ugumu kutoka Simba ambayo ilimuuza Al Ahly kwani kwa mujibu wa mkataba aliosaini kama atatakiwa kurudi kucheza Tanzania basi timu anayoruhusiwa na Simba pekee ikiwa atakuwa bado ndani ya mkataba.

Kiliongeza kuwa mabosi wa Yanga wanapambania hivi sasa kuipata saini ya kiungo huyo raia wa Msumbiji ambaye amepoteza nafasi ya kudumu katika kikosi cha Al Ahly alichojiunga nacho msimu uliopita.

“Luis amekubali ofa nono ya fedha ambayo amewekewa na uongozi wa Yanga ili kufanikisha usajili wake katia dirisha dogo lililofunguliwa wiki iliyopita.

“Amewekewa mkataba wa miaka mitatu wa kuusaini, lakini hivi sasa viongozi wanapambana kuhakikisha wanampata kiungo huyo, licha ya kuwepo ugumu wa mkataba wake Simba kabla ya kumuuza kwenda Al Ahly.

“Baada ya mchezaji mwenyewe kukubali, mabosi wa Yanga wamekubali kutoa fedha zote kwa pamoja na sio nusu nusu kama inavyoelezwa. Hivyo wanasubiriwa Ahly wafanye maamuzi, lakini kila kitu kipo tayari kwa Luis,” kilisema chanzo hicho.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said alisema kuwa: “Kama uongozi tupo tayari kumsajili yeyote atakayependekezwa na kocha wetu Nabi (Nasreddine) kwa gharama yoyote ya usajili.

“Na katika dirisha hili dogo tumepanga kusajili mchezaji mmoja bora Afrika ambaye tutatumia aina yetu ileile ya utambulisho kupitia mitandao ya kijamii na safari hii huenda ikawa alfajiri,” amesema Hersi.

Previous articleMABINGWA WAPYA WA KOMBE LA MAPINDUZI NI MLANDEGE
Next articleNIDHAMU IWE NA MWENDELEZO KWENYE LIGI KUU BARA