Home Sports JEMBE JIPYA MTIBWA SUGAR LATIMIZA NDOTO

JEMBE JIPYA MTIBWA SUGAR LATIMIZA NDOTO

 INGIZO jipya ndani ya Mtibwa Sugar, Vitalis Mayanga ameweka wazi kuwa ilikuwa ni ndoto yake kujiunga na Mtibwa Sugar alipoanza soka la ushindan.

Hivyo kujiunga na timu hiyo ametimiza ndoto yake ya muda mrefu.

Mayanga alitambulishwa rasmi kuwa ni mali ya Mtibwa Sugar Januari 11,2023.

Ni ingizo jipya ambapo alikuwa anakipiga ndani ya Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera.

Aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Ndanda na aliwahi kupata dili la kusaini Simba kisha akaibuka ndani ya KMC.

Wakati timu hiyo ikiambulia sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu Januari 13,2023 alianzia benchi.

Previous articleMUSONDA NI KIJANI NA NJANO
Next articleMABINGWA WAPYA WA KOMBE LA MAPINDUZI NI MLANDEGE