Home Sports MUSONDA NI KIJANI NA NJANO

MUSONDA NI KIJANI NA NJANO

RASMI uongozi wa Yanga umemtambulisha nyota mpya ndani ya kikosi hicho Kennedy Musonda raia wa Zambia kuwa mali ya timu hiyo.

Mshambuliaji huyo anaungana na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kwa ajili ya kupambania malengo ya timu hiyo.

Anatajwa kupewa dili la miaka miwili kwa ajili ya kutimiza majukumu ya Yanga ambayo ina kibarua cha kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho.

Anaungana na Fiston Mayele ambaye ni mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Yanga akiwa ametupia mabao14 msimu huu wa 2022/23.

Previous articleSIMBA YAPOTEZA DUBAI
Next articleJEMBE JIPYA MTIBWA SUGAR LATIMIZA NDOTO