Home International SIMBA YAPOTEZA DUBAI

SIMBA YAPOTEZA DUBAI

 KIKOSI cha Simba leo Januari 13,2023 kimeambulia kichapo cha bao 1-0.

Ni katika mchezo wa kirafiki ambapo wamepoteza dhidi ya Klabu ya Al Dhafra FC baada ya dakika 90.

Kikosi cha Kwanza Cha Kocha Mkuu Robert Oliviera langoni alianza Aishi Manula Kwa upande wa ulinzi ni Shomari Kapombe,Joash Onyango, Kennedy Juma.

Viungo ilikuwa ni Jonas Mkude, Pape Sakho, Sadio Kanoute,Clatoua Chama na Saidi Ntibanzokiza.

Ni John Bocco alianza upande wa ushambuliaji huku Kibu Dennis yeye alianza benchi.

Previous article32 BORA SIMBA, YANGA NA AZAM WAWAJUA WAPINZANI WAO
Next articleMUSONDA NI KIJANI NA NJANO