Home Sports USAJILI WA YANGA KUITIKISA NCHI, ALLY KAMWE ATAMBA

USAJILI WA YANGA KUITIKISA NCHI, ALLY KAMWE ATAMBA

OFISA Habari wa Yanga, Ally Kamwe, amefunguka kwamba, kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa Januari 15, mwaka huu, watatikisa nchi kwa usajili mkubwa watakaofanya.

Usajili wa dirisha dogo ulifunguliwa Desemba 16, 2022 na unatarajiwa kufungwa Januari 15, 2023, huku Yanga ikiwa tayari imemsajili kiungo, Mudathir Yahya.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kamwe alifunguka kuwa: “Kwa sasa tunaendelea kuboresha kikosi chetu baada ya kuwaongeza mkataba nyota ambao ni muhimu akiwemo Diarra (Djigui) na Aucho (Khalid), tutaendelea kuboresha mikataba kuendana na ripoti ya benchi la ufundi.

“Kwa upande wa kusajili wachezaji wapya, hatujaishia kwa Mudathir Yahya, bado tunaendelea na mipango ya kuongeza nguvu mpya zaidi ndani ya kikosi chetu.

“Kabla ya dirisha dogo kufungwa, klabu yetu ya Yanga itatikisa nchi, tutafanya usajili mkubwa ambao haujawahi kutokea, hivyo Wanayanga pamoja na wadau wote wa soka wasubiri kuona historia nyingine ikiwekwa na klabu hii.”

Previous articleSIMBA KAMBI YA KISHUA DUBAI,AKPAN NA OKWA WAACHWA
Next articleSIMBA YASHUSHA STRAIKA WA KAZI