LIVERPOOL WASHINDA KWA ZAWADI YA MABAO

MABAO mawili ya kujifunga kutoka kwa nyota Wout Faes yaliisaidia Liverpool kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Leicester.

Ushindi huo unaifanya timu hiyo kushika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu ya England.

Hii ni mechi ya kwanza ya Liverpool ikiwa Uwanja wa Anfield baada ya Kombe la Dunia na timu hiyo ilianza vibaya dakika ya nne tu baada ya Kiernan Dewsbury-Hall kumtungua Alisson.

Ni beki wa kati wa Leicester, Faes aliipatia Liverpool msaada, alitumia krosi ya Trent Alexander-Arnold  dakika ya 38 na ule wa pili ilikuwa dakika ya 45.

“Ni jinamizi kabisa kwake na jinamizi kwa Leicester,” alisema Jamie Carragher wa Sky Sports kwenye maoni yake – mmoja wa wachezaji wengine watatu kuwa na rekodi mbaya ya kufunga mabao mawili ya kujifunga mwenyewe katika mechi ya Ligi ya Kuu England.