Home Sports YANGA KAMILI KUIVAA MTIBWA SUGAR

YANGA KAMILI KUIVAA MTIBWA SUGAR

KUELEKEA mchezo wa kesho kati ya Mtibwa Sugar v Yanga benchi la ufundi la vinara wa ligi limeweka wazi kuwa lipo tayari.

Yanga imekuwa na mwendo wake bora ndani ya ligi ikiwa imetoka kupata ushindi kwenye mchezo dhidi ya Azam FC wa mabao 3-2.

Kesho Desemba 31 ina kazi ya kusaka pointi tatu dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Manungu.

Kocha wa Yanga, Soud Slim ameweka wazi kuwa wamefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mchezo wa kesho.

“Tumefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mchezo wa kesho na wachezaji wapo tayari kusaka ushindi

“Mpira unachezwa katika hali zote, sisi tumeiandaa timu yetu vizuri katika hali zote, iwe jua iwe mvua tutahakikisha tunafanya vizuri,” .

Miongoni mwa wachezaji ambao wataukosa mchezo wa kesho ni pamoja na Khalid Aucho, Feisal Salum na kiungo Bernard Morrison mwenye matatizo ya kifamilia.

Previous articleSIMBA 1-1 PRISONS
Next articleSIMBA YAPIGA KIFURUSHI, MANULA KATUNGULIWA