Home Sports SIMBA 1-1 PRISONS

SIMBA 1-1 PRISONS

UBAO wa Uwanja wa Mkapa dakika 45 zimekamilika ukisoma Simba 1-1 Tanzania Prisons.

Uzembe wa kipa namba moja wa Simba, Air Manula kwenye kuokoa mpira wa hatari uliopigwa na Kimenya umeigharimu timu yake.

Pongezi kwa mfungaji Jeremia Juma ambaye alikuwa kwenye eneo akiwa ametulia kama maji kwenye mtungi akamchagulia eneo la kumtungua Manula ambaye alikuwa ametoka.

Bao la Simba limefungwa na nahodha John Bocco kutokana na pasi ya Ntibanzokiza.

Pongezi kwa kipa namba moja wa Prisons , Hussein Abel ambeye licha ya kutunguliwa bao moja kaokoa michomo hatari zaidi ya Manula.

Uzembe wa Samson Mbangula umemfanya aonyeshwe kadi nyekundu kwa kumchezea faulo hatari Inonga ambaye amekwama kuendelea na mchezo wa leo.

Aishi Manula mechi ya tatu sasa anatunguliwa tu akiwa langoni.

Previous articleHIKI HAPA KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA PRISONS, NTIBANZOKIZA NDANI
Next articleYANGA KAMILI KUIVAA MTIBWA SUGAR