Home Sports SIMBA YAPIGA KIFURUSHI, MANULA KATUNGULIWA

SIMBA YAPIGA KIFURUSHI, MANULA KATUNGULIWA

KIKOSI cha Simba kimeibuka na ushindi wa mabao 7-1 Prisons katika mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Ni mabao ya ya nahodha John Bocco ambaye alitumia pasi ya Saidi Ntibanzokiza dakika ya 12,alifunga bao lingine dakika ya 46 na 62.

Shukrani kwa Ntibanzokiza ambaye alifunga mabao matatu pia kwenye mchezo wake wa kwanza akiwa na uzi wa Simba dakika ya 60,64 na 69 na ule msumari wa nne ulipachikwa na Shomary Kapombe dakika ya 88.

Hussein Abel kipa namba moja wa Prisons alikuwa na wakati mzuri kipindi cha kwanza kwa kuokoa michomo lakini bahati haikuwa yake kipindi cha pili.

Bao la dakika ya 62 alilofungwa na Bocco katika harakati za kuokoa mpira alikwama kuupeleka mbali mpira ukakutana na kichwa cha Bocco.

Ni Aishi Manula kipa namba moja wa Simba hakuwa kwenye ubora wake kipindi cha kwanza kwa kufungwa bao dakika 20 katika harakati za kuokoa krosi ya Jeremia Juma.

Hii inakuwa ni mechi yake ya tatu Manula anaonja joto ya kutunguliwa bao mojamoja akiwa langoni.

Previous articleYANGA KAMILI KUIVAA MTIBWA SUGAR
Next articleCHAMA CHA WATU WENYE UALBINO- TAS WAPATA MSAADA WA VIFAA