Home Sports WAARABU WAMFUATA AZIZ KI YANGA SC

WAARABU WAMFUATA AZIZ KI YANGA SC

IMEFAHAMIKA kuwa matajiri wa Klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco wamefunga safari na kuja nchini kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya kumpata kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mburkinabe, Stephane Aziz Ki.

Hiyo ni mara ya pili kwa Berkane kumfuata kiungo huyo kwa ajili ya mazungumzo ya kuinasa saini yake tangu akiwa katika klabu yake ya zamani ya Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast.

Yanga iliingia katika vita kali ya kuwania saini ya kiungo huyo dhidi ya Berkane katika usajili mkubwa wa msimu huu kabla ya kushinda na kiungo huyo kuvalia jezi zenye rangi ya njano, kijani na nyeusi.

Mmoja wa mabosi wa Yanga, ameliambia Championi Jumatano kuwa, wapo wachezaji wengi wanawaowaniwa na baadhi ya klabu za ndani na nje na kati ya hao ni Aziz Ki mwenye kiwango bora hivi sasa.

Bosi huyo alisema kuwa Berkane tayari wametuma ofa kwa uongozi wa Yanga kabla ya mabosi wao kutua nchini kwa ajili ya kutua kukamilisha usajili wake kama wakipewa majibu mazuri.

Aliongeza kuwa licha ya kutuma ofa hiyo Berkane, upo ugumu wa Yanga kumuachia kiungo huyo kutokana na umuhimu mkubwa alionao katika kuelekea hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

“Ukiona ofa nyingi zinakuja katika timu kwa baadhi ya wachezaji wako kuhitajikana klabu nyingine kubwa Afrika, basi ujue una kikosi bora.

 

Previous articleKARIBU KWENYE FAMILIA YA KIBINGWA YA MERIDIANBET UFURAHIE SLOTI YA BURSTING HOT 5
Next articleKAKOLANYA ATAJWA AZAM FC