Home Sports SIMBA YAKUSANYA FURUSHI LA POINTI KANDA YA ZIWA

SIMBA YAKUSANYA FURUSHI LA POINTI KANDA YA ZIWA

KWENYE msako wa pointi 9 kanda ya Ziwa kikosi cha Simba kimegotea kwenye pointi 7 baada ya kuyeyusha pointi mbili.

Furushi la pointi 7 wanarejea nazo Dar wakiwa nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zao ni 41 vinara ni Yanga wenye pointi 47 wote wamecheza mechi 18.

Ni mechi tatu Simba chini ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda imecheza ugenini ambapo ilikuwa Uwanja wa Kirumba, Geita Gold 0-5 Simba, Kagera Sugar 1-1 Simba Uwanja wa Kaitaba.

Ule mchezo wa tatu ulikuwa Uwanja wa Kirumba ubao ulisoma KMC 1-3 Simba.

Safu ya ulinzi ya Simba imeokota nyavuni mabao mawili huku ile ya ushambuliaji ikitupia mabao 11.

Ni beki Henock Inonga yeye katupia kwenye mechi mbili mfululizo kanda ya Ziwa, aliwatungua Kagera Sugar na KMC.

Kikosi cha Simba kinatarajiwa kurejea leo Dar na miongoni mwa mastaa ambao wapo kwenye msafara huo ni pamoja na Gadiel Michael, Sadio Kanoute, Said Ntibanzokiza, Aishi Manula, Pape Sakho na Clatous Chama.

Previous articleMZEE WA MAKOROKOCHO AJIBU KUIBUKIA SINGIDA BIG STARS
Next articleKIPA SIMBA SC AINGIA ANGA ZA AZAM FC