Home Sports ALI AHAMADA ATUNGULIWA MBILI CHAP KWA HARAKA

ALI AHAMADA ATUNGULIWA MBILI CHAP KWA HARAKA

MOJA ya sehemu ambazo Azam FC wanapaswa kuboresha pia kwa sasa kwenye usajili wa dirisha dogo ni upande wa mlinda mlango kutokana na makosa mengi anayoyafanya akiwa langoni.

Weka kando mechi ya leo dhidi ya Yanga ambayo amefungwa mabao mawili ndani ya dakika mbili kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union aliruhusu mabao ambayo yaliipa tabu timu yake kusaka ushindi.

Ni dakika 45 ubao wa Uwanja wa Mkapa unasoma Azam FC 1-2 Yanga ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.

Ni Sopu alianza kumtungua Diarra kisha Yanga wakajibu mapigo kupitia kwa Fiston Mayele na Aziz KI.

Previous articleSOPU KAANZA KUIKABILI YANGA KWA MKAPA
Next articleAZAM FC YATUNGULIWA SOPU AKITUPIA MBILI